Molinga: Siondoki Yanga, Labda Waniache – Video

BILA shaka kwa mpenda soka yeyote kwa sasa angetamani zaidi kujua malengo ya wachezaji mbalimbali wa hapa nchini na hata nje ya nchi.Wachezaji wengi kwa sasa wapo makwao wakiwa wanajipanga kuhakikisha wanarejea kwenye ligi baada ya kusimama kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.

 

Pale kwenye kikosi cha Yanga kuna mshambuliaji David Molinga ‘Falcao’ ambaye unaweza kusema kuwa ndiye bora zaidi kuliko wengine wote akiwa hadi ligi inasimama alikuwa amefanikiwa kufunga mabao tisa kwenye timu hiyo.

 

Mabao nane ameyafunga kwenye Ligi Kuu Bara mabao nane na moja katika Kombe la Shirikisho (FA) ambapo Yanga wapo hatua ya robo fainali.

Hakuna mchezaji mwingine ambaye ameweza kufunga kiwango hicho cha mabao kwenye kikosi cha Yanga, leo Championi Jumatano limefanya naye mahojiano baada ya kumkuta ufukweni akijifua ili kufahamu mambo mengi kumhusu.

 

Ikumbukwe tu kwamba Molinga alijiunga na Yanga, mwanzoni mwa msimu huu, akitokea kwenye Ligi Kuu ya nchini kwao Congo, akiwa ni chaguo la kwanza la aliyekuwa kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera.

 

UNAISHI VIPI KIPINDI HIKI CHA CORONA?

“Kusema kweli kwangu kipindi hiki cha mapumziko ya Virusi vya Corona, nilikuwa nimekaa tu nyumbani zaidi nilikuwa nazingatia kufanya mazoezi ya viungo, tukisubiria maelekezo mapya kutoka kwa viongozi wetu wa timu, maana wao ndiyo wanafahamu zaidi kinachoendelea kwenye mamlaka zaidi ya Ligi Kuu Bara.

 

KWA NINI UMEAMUA KUJA KUJIFUA HAPA UFUKWENI?

“Leo nimeona nianze rasmi mazoezi ya mpira baada ya jana (Juzi Jumapili), kumsikia rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akisema kuwa kuna uwezekano wa ligi kurejea ndani ya wiki hata nje ya nchi.Wachezaji wengi makwao wakiwa David Molinga ‘Falcao’ alikuwa amefanikiwa Ligi Kuu Bara mabao Kombe la Shirikisho (FA) ambapo Yanga wapo hatua Hakuna mchezaji mwingine ambaye ameweza kufunga kiwango hicho cha mabao kwenye kikosi cha kwenye hii, hivyo nikaona ni vyema nikaanza kufanya mazoezi ya kucheza mpira ili nitakapokutana na wenzangu nisihangaike kwenye suala la kucheza maana sijafanya mazoezi kabisa.

 

UNAMAANISHA KWA KIPINDI CHOTE HUKUWAHI KUFANYA MAZOEZI?

“Ndiyo, kwa muda wote huo mimi niliamua kukaa tu nyumbani kwani pale kwangu nina vifaa takribani vyote vya mazoezi ya gym na viungo, hivyo nilikuwa nimejipangia ratiba tu kwamba leo nikiamka nitafanya hiki au kile ili tu kutimiza program nilizoachiwa na kocha wetu.

 

UKIFUNGA MABAO MANGAPI NA MALENGO YAKO NI YAPI?

“Kabla ya ligi kusimama nilikuwa na mabao nane ya ligi na moja ni la FA, kuhusu nina malengo ya kumaliza ligi na mabao mangapi mimi nadhani hilo ni suala la kumuomba Mungu tu kwani yeye ndiye anafahamu nitafunga mangapi hadi msimu unaisha. “Zaidi tuombe ligi ianze nikiwa mzima nitafanya vizuri maana mimi ni mchezaji ninayejiamini.

 

NINI TOFAUTI YA LIGI YA CONGO NA TANZANIA?

“Tofauti ipo kubwa maana Ligi ya hapa Tanzania ina mashabiki wengi tofauti na Congo, maana hapa kuna muda tunaenda mkoani tunaona watu wanajitokeza kwa wingi zaidi tofauti na Congo, jambo linalonivutia sana.

 

UKIWA CONGO ULIKUWA UNACHEZA TIMU GANI?

“Congo nilikuwa nachezea timu moja inaitwa FC Renaissance du Congo, ambayo niliitumikia kwa miezi sita tu kabla ya kuja huku, maana kabla ya kuungana nayo nilikuwa nje ya dimba nikisumbuliwa na majeraha yaliyonichukua muda mrefu, hivyo pale nilicheza kama sehemu ya kujiweka fi ti tu ili nije kucheza huku.

 

MATARAJIO YAKO MSIMU UJAO, UTABAKI YANGA AU UNAONDOKA?

“Mimi sitarajii kuondoka Yanga sasa hivi, maana imeshakua ni moja ya familia yangu, hivyo suala la kuondoka litakuja tu pale wao wakitaka niondoke, zaidi nitasikilizia hadi nitakapomaliza mkataba wangu

 

MAKAZI YAKO RASMI NI CONGO AU UFARANSA?

“Familia yangu kwa maana ya mke na watoto wangu wote wanaishi Ufaransa, ila maisha yangu mimi huwa nachanganya kwa maana huwa naishi Congo na mara nyingine Ufaransa ambako familia yangu ipo kwa sasa,” alisema Molinga.

DAR ES SALAAM,TanzaniaMUSA MATEJAMakala – Bongo

RC MAKONDA “FUNGUENI HOTEL, WOTE MLIOKIMBIA RUDINI TUPIGE KAZI”


Loading...

Toa comment