Moloko Aanza Tambo Yanga

WINGA machachari wa Yanga, Jesus Moloko, anataka kuona akiendelea kufunga mabao katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara ili kuhakikisha wanabeba taji hilo.

Hiyo ni siku chache tangu atoke kufunga bao katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Geita Gold kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza na Spoti Xtra, Moloko alisema anataka kuifungia timu yake mabao kwa lengo la kuipa ubingwa wa ligi.

Moloko alisema kuwa anafahamu haitakuwa kazi nyepesi kwake kufunga katika kila mchezo, lakini atajipanga vema kushirikiana na wenzake kufanikisha malengo hayo.

“Binafsi nitafurahi kuona ninaendelea kuifungia timu yangu mabao katika michezo ijayo ya ligi ili kufanikisha malengo ya timu msimu huu.

“Malengo yetu sisi wachezaji, benchi la ufundi na viongozi ni kuchukua ubingwa wa ligi msimu huu.

“Ili hayo yafanikiwe ni lazima kila mchezaji atimize majukumu yake, mimi nimepanga kutimiza majukumu yangu ya kufunga na kutengeneza nafasi za kufungwa kwa wenzangu,” alisema Moloko.

~~WILBERT MOLANDI, Dar2181
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment