Moloko Apewa Mikoba ya Carlinhos Yanga

WINGA mpya ndani ya Yanga, Jesus Moloko, amekabidhiwa rasmi mikoba ya Carlos Carlinhos katika suala zima la kupiga mipira iliyokufa.

 

Msimu uliopita, Carlos Carlinhos ambaye aliomba kusepa ndani ya kikosi cha Yanga kabla ya msimu haujamalizika, alikuwa na jukumu la kupiga mipira iliyokufa na katika pasi zake tatu za mabao alizotoa, zote zilikuwa kwa mipira ya kona.

 

Juzi wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa, Dar ukisoma Yanga 0-1 Rivers United, nyota huyo alionekana akipipiga kona nyingi za Yanga jambo linalomaanisha kwamba mikoba ya Carlinhos kapewa yeye.

 

Yanga ilipata jumla ya kona 7 katika mchezo huo na Moloko aliweza kupiga kwa asilimia kubwa ikiwa ile ya dakika ya 37 ambayo ilileta kashikashi kwenye lango la Rivers United. Licha ya Yanga kupata kona nyingi, huku wapinzani wao wakipiga moja, walishindwa kutumia nafasi hiyo.

 

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam


Toa comment