MONA, MWANAYE WAANGUA KILIO HADHARANI

 

Yvonne Cherry ‘Mo­nalisa’ na mtoto wake Sonia George

MUIGIZAJI wa kitambo kwenye tasnia ya filamu Bongo, Yvonne Cherry ‘Mo­nalisa’ na mtoto wake Sonia George juzikati waliangua kilio hadha­rani walipokuwa wakikabidhi misaada kwenye kituo cha kulea watoto yatima cha Yoko kilichopo Mbezi- Mwisho jijini Dar.  Msanii huyo na mwanaye walitoa ma­chozi hayo huku watoto wa kituoni hapo nao wakilia kwa uchungu wakati mmoja wa wanafunzi wenzake na Sonia akitoa maelezo jinsi walivyofanikisha zoezi hilo.

Aliyeanza kulia ni mtoto wa staa huyo, Sonia baada ya kupewa kipaza sauti azungumze ambapo alishindwa, akaanza kulia huku mama yake akimkumbatia, wakajikuta wakilia pamoja.

“Masikini Sonia, anaonekana ana huru­ma na machozi yanamtoka kwa sababu na yeye anakumbuka amempoteza baba yake pia,” alisikika mwanafunzi mmoja aliyeongozana naye akisema.

Monalisa alizungumza na Ijumaa Wik­ienda na kusema kuwa ameamua kujitoa kusaidia wazo hilo la mtoto wake kwa sababu ameona anafanya jambo jema.

STORI ZOTE: Imelda Mtema

Loading...

Toa comment