The House of Favourite Newspapers

Monalisa Ang’ara Marekani

STAA wa filamu za Kibongo, Yvonne Cherrie ‘Monalisa’ ameng’ara nchini Marekani baada ya kuwa balozi wa Tamasha la Filamu za Kiafrika ‘Taff’ 2018 ambapo amepokea tuzo ya kumtambua kama balozi kutoka Tanzania alipohudhuria tamasha hilo lililofanyika juzikati Texas, Marekani.

 

Mona ameonekana kung’ara zaidi mwaka huu kwani tuzo hii ni ya pili kuipokea baada ya kupokea tuzo nyingine miezi mitatu iliyopita nchini Ghana, tuzo ya muigizaji bora wa kike Afrika.

Kwa hatua hiyo mama yake mzazi, Suzan Lewis ‘Natasha’ ametoa neno la kumshukuru Mungu na kueleza kuwa anafurahishwa na jinsi mwanaye anavyoendelea kuwa bora kila siku.

 

“Hii ni hatua nzuri sana, nimefurahi na naendelea kutoa neno la shukurani kwa Mungu kwa kuendelea kumpigania Monalisa kuwa bora kila siku na ni njia nzuri kwa wasanii wengine kuendelea kupambana kwani mwanya upo,” alisema Natasha.

STORI: Hamida Hassan

Comments are closed.