Monalisa Atwaa Ubalozi Bodi ya Filamu Nchini

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Dkt. Kiagho Kilonzo (kushoto) na Msanii wa Bongo Muvi, Yvon Cherry wakibadilishana mikataba baada ya msanii huyo kupewa dili la ubalozi wa bodi hiyo.

 

 

MSANII nguli wa filamu Tanzania, Ivon Cherry ‘Monalisa’ jana ametangazwa kuwa balozi wa kuitangaza Bodi ya Filamu Tanzania ili iweze kujulikana zaidi ndani na nje ya nchi.

Monalisa akishukuru baada ya kupewa ubalozi huo.

 

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar jana, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt, Kiagho Kilonzo amesema wameamua kuitangaza bodi hiyo ili kuweza kuongeza ufanisi katika kujulikana ndani na nje ya nchi.

Tukio likiendelea.

 

 

“Tulikutana na Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa tukazungumza na kuona kuna haja ya kuwa na balozi ndio tukaona Monalisa anafaa kuitangaza taasisi hii ambapo kupitia umaarufu wake ataitangaza katika shughuli zake za kila siku.

 

“Ataiongelea katika sehemu nne kwanza kupitia mitandao ya kijamii, kwenye matamasha, kwenye shughuli mbalimbali na kwenye vyombo vya habari na atakuwa mwenyeji wa wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi, “amesema Dkt Kilonzo.

 

Nae Balozi huyo mpya wa Bodi ya filamu Tanzania, Chery ‘Monalisa’ kwa upande wake baada ya kupewa heshima hiyo na kusainishana mkataba na bodi hiyo amesema ameishukuru bodi ya filamu kwa kumpa ubalozi wa kuitangaza.

 

“Nimekuwa mdau wa filamu kwa takribani miaka ishirini kwa hivyo basi wao wameona ninafaa katika kuitangaza na kuongelea taasisi na katika shughuli zake za kila siku niseme tu wamechagua mtu sahihi nimeiwakilisha Tanzania nje na ndani ya nchi kwenye filamu na nimeshawishi watu wengi kuingia kwenye tasnia hii” amesema Monalisa.

 

Mkataba huo umeanza desemba 7 mwaka huu ambapo bodi ya filamu pamoja na Monalisa wamesainiashana  hati ya maridhiano ya kuitangaza bodi hiyo.

 


Toa comment