The House of Favourite Newspapers

Monalisa Baada ya Mwanae Kufaulu Kaongea “Baba Ake Kafariki” -Video

Kitu pekee kinachompa faraja mzazi ni kuona maendeleo ya mtoto wake siku hadi siku hususani kwenye masomo, ndivyo ambavyo Muigizaji Monalisa ameshindwa kuzizuia hisia za furaha alizonazo baada ya mtoto wake wa kwanza anayeitwa Sonia kufaulu kidato cha nne kwa kiwango cha juu kabisa (Division One) huku akiwa na alama ‘A’ kwenye somo la Hesabu.

 

Global TV imepiga stori na Monalisa na kuelezea jinsi alivyopokea taarifa za ufaulu huo wa mwanae na mwenendo mzima wa mtoto wake huyo ambaye Baba yake alifariki miaka kadhaa iliyopita.

Comments are closed.