The House of Favourite Newspapers

MONDI AONYWA REKODI YA KUCHEZEA WANAWKE

0

WAKATI lile penzi shatashata la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mzazi mwenzake, Tanasha Donna Oketch, likidaiwa kupumulia mashine, jamaa huyo ameonywa. Diamond au Mondi ameonywa juu ya tabia yake ya ‘kuchezea’ wanawake kingono kwa ahadi ya ndoa kisha kuwaacha solemba.

TETESI ZA TANASHA

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, penzi la Mondi na Tanasha limekuwa likipita kwenye milima na mabonde huku madai mazito yakielekezwa kwa mama mzazi wa jamaa huyo; Sanura Kassim ‘Mama D’ kuwa, hamkubali mkwewe huyo.

“Ukitaka kujua kuna shida, wewe jaribu kumuuliza Mama Dangote (jina analotumia Mama D kwenye mitandao ya kijamii), jambo lolote kuhusu Tanasha uone majibu yake. “Lazima atakupa majibu yenye maswali, hawezi kukujibu vizuri kwa sababu hawana maelewano mazuri,” alisema mtu wa karibu wa familia ya Mondi.

WAPO WALIOKULA KIAPO

Tangu wawili hao watangaze kufunga ndoa, wapo watu waliokula kiapo kwamba, ndoa hiyo haitafanikiwa. Hivyo kufifisha ndoto ya wawili hao kuoana ambapo siku zinakatika tu na hawana tena mipango.

Zaidi sana, sasa kuna madai mapya kwamba, Mondi yupo njiani kuibuka na kifaa kipya ambapo swali limekuwa ni kutoka nchi gani kwani tayari amepita nchi tatu za Afrika Mashariki yaani Tanzania, Kenya na Uganda (Takeu).

“Kiukweli kwa sasa sioni dalili ya Mondi (Diamond) kumuoa Tanasha kwa sababu ‘wapinzani’ wamekuwa ni wengi akiwemo mama yake. “Sikufichi, Diamond ameshajua kwamba alipotea njia ‘so’ anatafuta mahali pa kutokea,” kiliendelea chanzo kumwaga nyepesinyepesi.

MONDI SIYO WA KUOA LEO WALA KESHO

Kufuatia hali hiyo, gazeti hili lilimtafuta Mondi kujua msimamo wake kwa sasa, lakini simu yake ya kiganjani haikupokelewa na hata alipotumiwa ‘chatting’ kwenye WhatsApp hakujibu.

Lakini siku chache zilizopita kabla ya kuwa na Tanasha, mmoja wa waandishi wetu alimbana Diamond kuhusu kumuoa Tanasha ambaye alijibu kwa kifupi: “Mimi siyo wa kuoa leo wala kesho.”

SHEHE AMUONYA

Hata hivyo, gazeti hili lilizungumza na shehe maarufu wa Taasisi ya Irshaad nchini; Shehe Ahmed Kandauma juu ya madai ya Mondi ya ‘kuchezea’ wanawake kingono na kuwaacha kama ni sahihi kwa kijana wa Kiislam ambapo alikuwa na haya ya kusema;

“Hakuna mwanamke anayependa kuchezewa na wanaume, labda tu kama anafanya hivyo katika juhudi zake za kujikwamua kiuchumi. “Lakini pale mwanamke anapokuwa katika harakati za kutafuta mwanaume ambaye kama mambo yakiwa mazuri wafunge ndoa, ni vyema akajiepusha na wanaume vicheche wanaotongoza wanawake kwa lengo la kustarehe na kumaliza matamanio yao ya ngono.

“Wakati mwingine mwanaume mwenye tabia ya kuchezea wanawake, anaweza kumfuata mwanamke ambaye ametamani mwili wake na kujifanya eti amebadilika na kuwa mtakatifu, jambo ambalo ni baya na ni dhambi katika Dini ya Kiislam.

“Anaweza kujiweka katika mazingira yanayoonesha kwamba amebadilika ili kumvuta mwanamke. Hapa lazima mwanamke ashtuke, jasiri haachi asili! Atakutumia kisha kukutupilia mbali.

“Wanaume wenye tabia hizo ni vigumu kubadilika. Inahitaji subira ya hali ya juu kujiridhisha kama kweli amebadilika au anazuga ili apate anachokitaka, hivyo hata hao wanawake nao ninawaonya,” alisema shehe huyo.

Baba D atia neno Akizungumzia tabia hiyo ya mwanaye ya kuchezea wanawake, baba mzazi wa Mondi; Abdul Juma ‘Baba D’ alisema kuwa, ukoo wao ni wa watu watanashati, hivyo suala la wanawake kuvutiwa nao hilo liko wazi, lakini si kweli kwamba tabia hiyo ya kuchezea wanawake amerithi kutoka kwake.

TUJIKUMBUSHE

Mara kadhaa Mondi amekuwa akijinasibu kuwa amekuwa ‘akiwatafuna’ warembo mbalimbali maarufu kwani kabla ya kuwa staa, walikuwa wakimdharau na kumuita majina ya ajabuajabu.

Anasema kuwa, baada ya kupata umaarufu na mkwanja, kweli ameamua kuwapitia warembo tofauti ili kukamilisha furaha ya moyo wake kwani ni ndoto aliyokuwa akiiota siku nyingi.

MSURURU WA WAREMBO

Mondi amekuwa na orodha ndefu ya warembo aliowahi kuwa nao kwenye uhusiano wa kimapenzi ambapo ni pamoja na;

Upendo Mushi, Rehema Fabian, Hawa wa Nitarejea, Irene Uwoya, Wema Sepetu, Hamisa Mobeto, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Tanasha, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Nuzrat.

Wengine ni Natasha wa Moyo Wangu, Jacqueline Wolper, Tunda Sebastian, Lyyn (Irene wa Kwetu), Najma, Hamisuu Malick na Kim Nana

Leave A Reply