Mondi Atajwa Vipengele 6 Tuzo za Afrima

WAANDAAJI wa Tuzo za AFRIMA 2021, wametangaza listi ya wasanii wa Bongo Fleva watakaowania tuzo hizo kwenye vipengele mbalimbali.

 

Kwenye listi hiyo msanii anayeongoza ni Kundi la Blaq Diamond kutoka Afrika Kusini ambao wametajwa kwenye vipengele nane.

 

Namba mbili inashikiliwa na Focalistic ambaye ametajwa kwenye vipengele saba na namba tatu inashikiliwa na Wizkid ambaye ametajwa kwenye vipengele sita.

 

Kwa upande wa Tanzania, listi hiyo inaongozwa kama kawaida na diamond Platnumz ambaye jina lake limetajwa kwenye vipengele sita.

 

Wasanii wengine waliotajwa ni Nandy, King Kiba, Harmonize, Darassa, Rosa Ree na Zuchu.

 

Kwa upande wa ma-DJ, Tanzania inawakilishwa na DJ Sinyorita kutoka Clouds FM huku watayarishaji wa muziki wakiwakilishwa na Lizer Classic na watayarishaji wa video wakiwakilishwa na Director Kenny.


Toa comment