MONDI KUPIGA BILIONI 3 SIKU 150

HARUFU ya ubilionea imeanza kumnyemelea staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ baada ya shoo zake kuonesha mafanikio ya kupiga hadi shilingi bilioni 3 ndani ya siku 150 tu.  Kwa mujibu wa chanzo cha karibu kilichozungumza na staa huyo anayetikisa na Wimbo wa Kanyaga, hivi sasa kwa shoo moja anaingiza si chini ya shilingi milioni 100.

“Mambo yake yamekuwa supa sana siku hizi. Kwa shoo moja tu iwe ndani au nje ya nchi anaingiza si chini ya shilingi milioni 100 na hiyo ni kwa siku moja tu.” Chanzo kilizidi kumwaga data kuwa, kwa sasa Diamond ana shoo mezani zisizopungua 30 ambazo ni za ndani na nje ya nchi na hapo bado anaendelea kupokea oda ya shoo nyingine hadi mwaka uishe.

“Ukitazama ratiba ya Diamond kuanzia sasa hadi mwaka uishe atakuwa ameshafanya shoo kama 30 hivi ndani ya miezi mitano ambayo ukihesabu kwa siku unapata sawa na siku kama 150 hivi,” kiliweka nukta chanzo hicho. Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Diamond ambaye alikiri kuwa na shoo hizo na kiasi cha pesa anachokipata kwa shoo.

“Hadi sasa nina zaidi hata ya hizo shoo 30 kwa hesabu ya harakaharaka na shoo zangu si za kitoto, napiga si chini ya milioni 100 kwa moja tu,” alisema Diamond kwa kifupi. Shoo za Diamond kwa mwezi Julai ameshafanya mbili mojawapo ni Tabora katika Wasafi Festival, tarehe 25 atakuwa Kampala Uganda, 27 atakuwa Mwanza na 28, Bujumbura Burundi.

Agosti 3, atakuwa Nosybe Madagascar, 7, Dodoma, 10 na 11, New York na Minnesota Marekani, 17, Kigali Rwanda, 24, London Uingereza na 31, New York. Septemba 7, atakuwa Berlin Ujerumani, Oktoba 5, Dar es Salaam, 11, 12 na 13, Toronto, Montreal na Edmonton, Canada. Novemba 15, Dubai na Desemba 7, Guinea Bisau.


Loading...

Toa comment