MONDI, TANASHA ILIKUWA NI PROJEKTI?

WAKATI Tanasha Donna Oketch anatambulishwa rasmi Novemba 23, mwaka jana kama mchumba halali na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Mondi’ katika Tamasha la Wasafi lililofanyika Mtwara, wengi waliona ndiyo mbadala wa mjasiriamali, Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’, raia wa nchi jirani ya Uganda. 

 

Nakumbuka, Mondi aliwahi kumfagilia kwa kusema; “Tanasha ni mwanamke pekee aliyenionesha yupo makini na ana sifa zote za kuingia naye kwenye ndoa na sasa ni rasmi ninatangaza kwamba ninamuo.

 

“Ana sifa zote ambazo mwanaume yeyote aliyekamilika angetamani awe mkewe. Sisi wanaume tulio wengi huwa tunaangalia shepu, maumbile, mvuto wa nje na mengineyo ambayo yote anayo. Lakini kikubwa zaidi kuliko vyote ni TABIA! Ana tabia nzuri.”

 

Baada ya kusema hivyo, ‘series’ ya projekti yao ikaanzia hapo kwa bidada huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye ni chotara wa Mkenya na Muitaliano, mwenye kuzungumza lugha Kingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kidachi na Kihispaniola.

AHAMISHWA MADALE

Kipindi Mondi anatoka na Zari alikuwa akiishi naye nyumbani kwa mama yake, Madale-Tegeta jijini Dar, lakini baada ya kumpata Tanasha alimhamisha makazi na kwenda kuishi naye pande za Mbezi-Beach kwa Zena jijini Dar. Siku chache mbele alimtambulisha mbele ya mama yake, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ pamoja na dada yake, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ wakiwa wanapata chakula cha mchana.

 

Kuanzia hapo, Tanasha ambaye pia ni mtangazaji wa Radio NRG ya Mombasa akawa anatinga Bongo kila wikiendi na siku za kawaida anakuwa Mombasa nchini Kenya akifanya kazi ya utangazaji.

ISHU YA KUOANA

Kuonesha kuwa kuna kitu kilikuwa nyuma yao, Mondi aliibuka na kusema kuwa anataka kufunga ndoa na Tanasha Siku ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ (Februari 14, mwaka huu) ambapo kama utakumbuka ndiyo siku ambayo alimwagana rasmi na Zari ambaye amezaa naye watoto wawili, mmoja wa kike, Latifah Nasibu ‘Princess Tiffah’ na wa kiume, Prince Nillan Nasibu.

 

Mondi alichochea zaidi kwa kusema kuwa, ndoa hiyo itahudhuriwa na watu maarufu akiwemo mwanamuziki Rick Ross kutoka nchini Marekani. Hata hivyo, ishu ilikuja kukwama ilipokaribia Valentine’s Day ambapo Mondi alisema ameamua kuisogeza mbele kutokana na harusi yao iwe nzuri na wahudhurie watu wengi maarufu.

WOTE KUTOA NGOMA

Wakati mashabiki wakiwa njia panda wasijue kama ndoa ipo au la, limeibuka moja baada jingine baada ya Tanasha kuibuka na kusema kuwa anatarajia kuachia wimbo wake wa kwanza Ijumaa hii.

Kuonesha hilo, tayari vipande vya video hiyo vimeanza kuachiwa na Mondi kupitia ukurasa wake wa Instagram.

 

Kwa upande wa Mondi, naye yupo chimbo akijiandaa kuachia wimbo wake mpya. Kumbuka kuwa, mara ya mwisho Mondi kuachia ngoma yake kama yeye ukiacha za kushirikishwa ilikuwa ni Juni, mwaka jana alipoachia Ngoma ya Baila inayopatikana kwenye albamu yake ya A Boy From Tandale.

 

Tangu hapo amekuwa akishirikishwa tu na wasanii wake katika ngoma mbalimbali kama Kwangwaru ya Hamornize, Jibebe akiwa na Lavalava na Mbosso pamoja na Tetema akiwa na Rayvanny.

Kwa ujio huu mpya wa Mondi na Tanasha katika muziki na ‘chembechembe’ za uhusiano tuelewe ilikuwa projekti ya muziki kwa kila mmoja?

Tusubiri!

Mwandishi wa makala haya anapatikana kwa simu: 0713 133 633, e-mail: nitumiehapa@gmail.com


Loading...

Toa comment