Morocco Vs Tanzania: Mchezo wa 16 Bora Unaotarajiwa Kushangaza Mashabiki

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2025, inayoendelea nchini Morocco ni kati ya michuano isiyotabirika zaidi katika historia ya hivi majuzi.
Tangu kuanzishwa kwa AFCON 1957 mashindano hayajakuwa wazi hali ya kwamba mataifa matano au sita yanaweza kuwania taji hilo kwa umakini.
Mbali na mwenyeji,Morocco, mataifa kadhaa ni miongoni mwa washindani wakuu: Senegal, Misri, Ivory Coast na Algeria, zote tayari zimefuzu kwa Kombe la Dunia la 2026.
Moja ya maajabu ya Kombe la Mataifa ya Afrika ni kutotabirika kwake.
Matoleo manane ya mwisho yameshuhudia mabingwa saba tofauti, huku Ivory Coast ikiwa ndiyo pekee iliyotawazwa mara mbili katika matoleo matano yaliyopita, mwaka wa 2015 na 2024.

Takriban nusu karne baada ya taji lao pekee la bara, Wamorocco wanaota ndoto ya ushindi kwenye ardhi ya nyumbani na katika mtoano wa 16 bora, watavaana na Taifa Stars ya Tanzania.
Chini ya kocha Walid Regragui, Morocco, taifa lililoorodheshwa juu zaidi barani Afrika katika viwango vya FIFA, lilifikia kilele cha kandanda ya dunia mnamo 2022, na kuwa timu ya kwanza ya Afrika kucheza nusu fainali ya Kombe la Dunia.
Simba wa Atlas imeingia katika mashindano hayo sio tu kwa fursa nzuri walio nayo nyumbani, lakini pia kwa dhamira ya kupata taji lao la pili la Ubingwa wa Mataifa ya Afrika tangu 1976. Jumapili tarehe 4 Januari watavaana na Taisa Stars; je unatabiri matokeo gani?
Stori na Elvan Stambuli, Global

