Morrison Alia Kuwakosa Yanga

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, amejikuta akitoa kilio kufuatia kutokuwa sehemu ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, inayotarajiwa kuchezwa Septemba 25, mwaka huu katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Morrison hatakuwa sehemu ya mchezo huo, kufuatia kuwa na adhabu ya kutocheza mechi tatu, baada ya kuvua bukta wakati akishangilia ushindi wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Morrison alisema: “Watu wengi wamesahau kama mimi sitakuwa sehemu ya mchezo huo wa Ngao ya Jamii, kutokana na kutumikia adhabu ila kungekuwa na uwezo wa kuomba adhabu isogezwe mbele ningeomba ili niwalambishe juisi Yanga, jambo ambalo halitawezekana tena japo tutashinda.”

MUSA MATEJA, Dar es Salaam


Toa comment