Morrison Ampa Jeuri Gomes

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amefunguka kuwa kurejea kwa kiungo mshambuliaji wake, Bernard Morrison hususani katika mchezo wao ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika ni miongoni mwa vitu vinavyowapa matumaini makubwa ya kufanya vizuri.

 

Baada ya ushindi wao wa kwanza tangu kuanza kwa msimu huu dhidi ya Dodoma Jiji, Simba wamerejea Dar es Salaam kujiandaa na karata yao ya kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo wataanzia ugenini kucheza dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

 

Gomes aliliambia Spoti Xtra kwamba: “Michezo mitatu iliyopita imekuwa ya faida kubwa kwetu kutuandaa na mashindano mbalimbali tutakayoshiriki mwaka huu, kwa namna ninavyokiona kikosi changu nashawishika kusema tupo tayari.

 

“Tuna mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika michuano ambayo ni muhimu kwetu, lazima tujiandae kufanya vizuri katika hatua hii na ni jambo zuri kuona tuna nafasi ya kumtumia tena Bernard Morrison katika mashindano hayo.”

JOEL THOMASA, Dar


Toa comment