The House of Favourite Newspapers

Morrison Ampiga Mkwara Mzito Kapombe, Atamani Ligi Ianze Wamalizane

0
Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Bernard Morrison

KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, raia wa Ghana, Bernard Morrison, ameahidi kuwagaragaza mabeki atakaokutana nao msimu ujao akiwemo beki wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe.

Morrison alijiunga na Yanga kwa mara ya kwanza, Januari 15, 2020 kabla ya mkataba wake kuleta mgogoro na baadaye Agosti 8, 2020 akatimkia Simba ambako amehama tena na kurudi Jangwani baada ya makataba wake kumalizika.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Morrison alisema kuwa, kufuatia uzito wa mazoezi anayoyafanya kwa sasa kwao nchini Ghana, ana uhakika beki yoyote atakayepangwa naye mara baada ya kurudi Bongo atamsumbua vibaya tofauti na walivyomzoea awali.

Beki wa Simba Shomari Kapombe

Aliongeza kuwa, anajinoa vikali kuhakikisha kuwa msimu ujao anakuwa zaidi ya alivyokuwa misimu iliyopita kwani anaamini katika mazoezi makali na sio vitu vingine.

 

“Ninafanya mazoezi huku Ghana ya kutisha sana, kiasi kwamba kama kocha atakuja kunipa nafasi ya kucheza mechi zijazo, basi mabeki nitakaokabana nao wajipange kutema damu.

Leave A Reply