The House of Favourite Newspapers

Morrison Aondolewa Kikosini Simba

0

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, ameondolewa kwenye kikosi cha timu hiyo kufuatia kuwa na matatizo ya kifamilia.

 

Morrison ambaye wikiendi iliyopita kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambao Simba walifungwa bao 1-0 alicheza dakika zote tisini, anatarajiwa kuukosa mchezo wa leo Jumapili dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Katika mazoezi ya jana Jumamosi yaliyofanyika Simba Mo Arena, Dar, na kushuhudiwa na Spoti Xtra, Morrison hakuwa sehemu ya mazoezi hayo ya mwisho kabla ya kuivaa Coastal Union leo Jumapili.

 

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, alisema: “Morrison hayupo na timu kwa sababu ya matatizo ya kifamilia, pia kuna wachezaji wengine watakosekana katika mchezo dhidi ya Coastal akiwemo Parfect Chikwende ambaye yupo na kikosi cha timu yao ya taifa.”

STORI: CAREEN OSCAR,Dar es Salaam

Leave A Reply