Morrison hatari yake ni baada ya dakika 118

MZEE wa kukera ndani ya ardhi ya Bongo, Bernard Morrison ambaye ni mali ya Simba kwa sasa akitokea Klabu ya Yanga, hatari yake inaonyesha ni kila baada ya dakika 118.

 

Morrison amekuwa mzee wa matukio pia akiwa Simba ambapo aliwahi kukumbana na adhabu ya kufungiwa mechi tatu na Kamati ya Masaa 72 kwa kitendo cha kupigana na mchezaji wa Ruvu Shooting, Juma Nyoso wakati ubao wa Uwanja wa Uhuru ukisoma Simba 0-1 Ruvu Shooting.

 

Pia hivi karibuni kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui FC, Uwanja wa Kambarage wakati ubao ukisoma Mwadui 0-1 Simba, alionekana na hatia ya kumvuta mwamuzi msaidizi jambo lililopeleka apewe onyo na Kamati ya Masaa 72.

 

Kwenye ligi amecheza mechi 16, amefunga mabao matatu na pasi nne za mabao, ametumia dakika 832 na kumfanya ahusike kwenye jumla ya mabao 7 kati ya 58 ambayo yamefungwa na timu hiyo.

 

Mechi zake ilikuwa mbele ya:- Ihefu, dk 67, Mtibwa Sugar, dk 66, Biashara United, dk 25, Gwambina FC, dk 23, JKT Tanzania, dk 13, Prisons, dk 90, Ruvu Shooting, dk 45, Coastal Union, dk 90, Polisi Tanzania, dk 61.Dodoma Jiji, dk 70, Azam FC, dk 20, Biashara United, dk 80, Prisons, dk 24, Mwadui, dk 45, Gwambina, dk 62 na Dodoma Jiji dk 51

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es SalaamTecno


Toa comment