The House of Favourite Newspapers

Morrison: Nimeshinda Tuzo ya Nguo Bora ya Ndani

0

WAKATI wachezaji John Bocco, Aishi Manula, Mohammed Hussein na Fei Toto na wengine wakiondoka na tuzo za TFF usiku wa kuamkia jana katika Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) msimu wa 2020/21, Benard Morrison anasema aliambulia kurudi na chupa ya maji nyumbani.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mchezaji huyo asiyeishiwa na vituko ameandika kuwa tuzo pekee aliyoshinda ni nguo bora ya ndani ya msimu.

 

“Kwa hivyo jana usiku wengine walipokwenda nyumbani na tuzo, mimi nilikwenda nyumbani na chupa ya maji, lazima nikuambie kabla ya kuanza kusema nimeshinda nguo bora ya ndani ya msimu, kila mtu alistahili hongera kwa wote”.

 

So last night as others went home with awards, I went home with UHAI bottle of water😂 I have to tell you before you start saying I won best chupi of the season🤦🏽‍♂️ Everyone deserved it so CONGRATS to them all💪🏾 

Leave A Reply