The House of Favourite Newspapers

ads

Moses Kaluwa Agomea Matokeo Uchaguzi Simba Afunguka Mazito, Agomea Kusaini

0

ADVOCATE Moses Kaluwa, aliyekuwa anawania nafasi ya Mwenyekiti wa Simba kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika juzi Jumapili, ameweka wazi kuwa, hajaridhishwa na matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Murtaza Mangungu.

Kaluwa alisema, ameshindwa kusaini karatasi ya kukubali matokeo hayo ya uchaguzi kwa kuwa hajakubaliana nayo, ingawa uamuzi wake huo hauwezi kubadilisha lolote.

Mangungu ameshinda uchaguzi huo na kutetea nafasi ya mwenyekiti kwa kupata kura 1,311, wakati Kaluwa akivuna kura 1,045 kwenye matokeo ya uchaguzi huo ambayo yalitolewa alfajiri ya jana Jumatatu na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Simba, Boniface Lihamwike.

“Sijaridhishwa na matokeo na sijasaini karatasi ya matokeo kuonesha kukubali kwa kuwa msimamo wangu upo wazi. Ila ombi langu kwenu ni kuwa Simba ni kubwa kuliko uchaguzi.

“Simba ni kubwa kuliko sisi, wote tunajukumu kubwa la kuijenga Simba, tunaipenda Simba, hatupendi watu. Hata kama sijasaini ila nitashirikiana na wenzangu.

“Zile sera na hoja zangu, walizisikia wanaweza kuzifanyia kazi na kuziboresha kama zitakuwa na mapungufu,” alisema.

STORI NA ISSA LIPONDA

JEZI za YANGA ZAWEKA REKODI, SIMBA WATOA TAMKO ZITO | KROSI DONGO

Leave A Reply