The House of Favourite Newspapers

Moses Phiri Aaga Rasmi Kwao Zambia, Awindwa na Simba na Yanga

0
Mshambuliaji wa Zanaco FC ya nchini Zambia, Moses Phiri.

 

MSHAMBULIAJI wa Zanaco FC ya nchini Zambia, Moses Phiri, rasmi ameaga ndani ya timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Zambia.

 

Phiri ambaye anawindwa na timu za Simba na Yanga, amekuwa katika kiwango bora ndani ya timu hiyo jambo ambalo limepelekea timu hizo kumuwania vikali.

 

Akizungumza na Spoti Xtra moja kwa moja kutoka nchini Zambia, meneja wa mchezaji huyo, Nyambe Nawa, alisema msimu ujao kuna asilimia kubwa kwa Phiri kucheza Tanzania baada ya kuhitajika na timu za Simba na Yanga.

 

“Simba na Yanga zote zinamuhitaji Phiri, hivyo mpaka sasa kuna asilimia kubwa sana kwake kucheza soka Tanzania msimu ujao, dirisha la usajili likifunguliwa kila kitu kitakuwa wazi,” alisema meneja huyo.

MARCO MZUMBE

Leave A Reply