The House of Favourite Newspapers

Moses Phiri Aionya Yanga Wapanga Kushinda Mataji Yote Msimu Huu

0

MSHAMBULIAJI wa Simba, Moses Phiri, amesema kwa mziki wa kikosi chao msimu huu, wamepanga kushinda mataji yote, huku wakianza na Ngao ya Jamii.

Phiri ambaye huu ni msimu wake wa pili ndani ya Simba, ameshuhudia msimu uliopita mataji yote ambayo ni Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho la Azam Sports na Ngao ya Jamii yakibebwa na Yanga, amesema msimu huu ni zamu yao, hivyo wapinzani wakae chonjo.

Wikiendi iliyopita, Simba ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa pili wa Ligi Kuu Bara ambapo Phiri alifunga bao moja likiwa ni la kwanza kwake msimu huu.

Kabla ya hapo, Phiri alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichobeba Ngao ya Jamii, michezo iliyochezwa Mkwakwani, Tanga, huku fainali wakiichapa Yanga kwa penalti 3-1, na kuivua ubingwa.

Akizungumza na Spoti Xtra, Phiri alisema: “Nafurahia kasi ambayo kikosi chetu kimeanza nayo msimu huu, ari ya ushindani kwenye kikosi ni kubwa na kila mmoja anajitoa kuhakikisha tunashinda mataji yote msimu huu.

“Tumeanza na Ngao ya Jamii, lakini tunataka kuhakikisha tunashinda na mengine, tunajua msimu huu utakuwa mgumu kutokana na kuongezeka kwa ushindani kutokana na ubora wa kila timu, lakini naamini katika ubora wa wachezaji waliopo na wale wapya tutafanya vizuri.”

STORI NA JOEL THOMAS

PATORANKING AFUNGUKA KUHUSU DIAMOND, ALIKIBA – ”WOTE ni MARAFIKI ZANGU, WATAKUWEPO KWENYE ALBAM”

Leave A Reply