The House of Favourite Newspapers

Moshi: Mzungu Ahukumiwa Jela Maisha kwa Madawa ya Kulevya

 

KILIMANJARO: Mahakama Kuu Kanda ya Moshi imemhukumu kifungo cha maisha jela mwanamuziki Christina Biskasevskaja (26) raia wa Lithuania kwa makosa ya kukamatwa  na madawa ya kulevya.

Christina alikamatwa Agosti 28, 2012 katika Uwanja wa Ndege KIA akijiandaa kuelekea Brussels Ubeligiji na madawa ya kulevya aina ya Heroin na Hydrochloride yenye uzito wa gramu 3775. 26 na thamani ya Tsh Mil 169,886,700.

Comments are closed.