The House of Favourite Newspapers

Mosimane Aamua Kupumzika Ukocha, Aahidi Kujikita Kukuza Soka la Afrika

0
Kocha mwenye mafanikio makubwa Barani Afrika Pitso Mosimane

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa miamba ya Soka Barani Afrika, Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini amesema baada ya kutumika kama kocha kwa miaka 21, sasa ameamua kupumzika ili kufanya mambo mengine nje ya ukocha.

Pitso Mosimane akiwafundisha vijana katika hafla ya wiki ya mwananchi

Pitso amesema hayo leo Ijumaa, Agosti 5, 2022 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam baada ya kukaribishwa na Klabu ya Yanga katika tamasha la Kilele cha Wiki ya Wananchi litakalofanyika kesho katika Dimba la Mkapa.

Mosimane amesema anapumzika kazi ya ukocha baada ya kuifanya kwa kipindi cha miaka 21

“Nikiwa kama Kocha kutoka Afrika nimefanya makubwa kwenye soka la Afrika na nina amini Afrika tuna nafasi ya kufanya zaidi ya nikichokifanya kwenye soka kukuza mpira wetu Ulimwenguni kote.

 

“Nilikuwa Uwanjani kila siku na mechi za mashindano zikiwa kila baada ya siku 3 na nilikuwa nasafiri sana, sasa nimeamua kupumzika na mapumziko yangu nayatumia kushiriki na Young Africans SC katika Wiki ya Wananchi,” amesema Pitso.

Leave A Reply