Nyumba Yateketea kwa Moto Keko – (Pichaz + Video)
MOTO mkubwa umeibuka na kuteketeza nyumba za watu na vibanda vya biashara katika maeneo ya Keko jijini Dar es Saalam alfajiri ya leo Alhamisi, Oktoba 1, 2020.
Baadhi ya familia zimepoteza makazi yao kutokana na moto huo ambao mpaka sasa chanzo chake bado hakijafahamika.
Aidha, juhudi za wananchi wa eneo hilo ndizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kuudhibiti moto huo licha ya madhara makubwa ya kuteketea kwa mali za wakazi hao na hakuna vifo wala majeruhi walioripotiwa.
Global TV Online imefika mpaka eneo la tukio na kujionea hali hiyo huku wananchi wakiendelea kumalizia kuuzima kwa kutumia maji na nyenzo nyingine za kuzimia moto.
Kulingana na mazingira halisi ya eneo hilo hakuna barabara ya moja kwa moja kufikia eneo ambalo moto huo umetokea.
View this post on Instagram