Moto wa Yanga waendelea Ligi Kuu, Mabao 68, Mzize Aongoza kwa Mabao 13!
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ni moto chini kwenye eneo la utupiaji mabao ndani ya msimu wa 2024/25.
Yanga SC baada ya mechi 26 safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Clement Mzize imetupia jumla ya mabao 68. Mzize ametupia jumla ya mabao 13 akiwa mzawa mwenye mabao mengi ndani ya ligi.
Ikumbukwe kwamba katika mabao hayo 68, Yanga imetupia mabao matano pekee kwa penati ambapo nne zilifungwa na Aziz Ki alifunga mabao manne akikosa penati mbili na pigo moja la penati lilifungwa na Pacome kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa KMC Complex.
Yanga SC rekodi zinaonyesha kuwa imekuwa na hatari zaidi ndani ya 18 ambapo safu yake ya ushambuliaji imetupia mabao 55 ikiwa eneo hilo huku mabao 13 wakifunga wakiwa nje ya 18.
Mbali na kuwa namba moja kwa timu yenye mabao mengi inaongoza ligi ikiwa na pointi 70 kibindoni mchezo wake ujao ni dhidi ya Namungo FC unatarajiwa kuchezwa Mei 13 Uwanja wa KMC Complex.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.