The House of Favourite Newspapers

Moto Wateketeza Jiji Zima la London

0

fire_painting1_700

Jiji Zima la London lilivyoteketea kwa moto.

Hebu vuta picha! Moto unaanzia kwenye jiko moja la kuchomea mikate kisha unashika kwenye majengo ya jirani! Kama masihara moto unazidi kusambaa, mara nyumba za mtaa mzima zinashika moto, harakati za kuuzima zinashindikana, unazidi kusambaa kwenye mitaa mingine na muda mfupi baadaye, jiji lote linateketea! Ni tukio la ajabu si ndiyo?

Basi kwa taarifa yako, tukio kama hilo limewahi kulikumba jiji kubwa na maarufu duniani la London nchini Uingereza!  Ilikuwaje?

Ilikuwa ni Jumapili ya Septemba 2, 1666 (mwaka unaohusishwa na shetani) ambapo moto ulilipuka kwenye kituo kimoja cha kuoka mikate kilichokuwa kikiitwa Thomas Farriner Bakery, Mtaa wa Pudding Lane jijini humo.

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

Jiji la London lilivyo sasa.

Muda mfupi baadaye, moto huo ulianza kusambaa kwenye majengo yaliyokuwa jirani na ‘bakery’ hiyo, kutokana na upepo mkali uliokuwa unavuma, moto uliendelea kusambaa kwa kasi kubwa kuelekea upande wa Magharibi mwa jiji hilo.

Licha ya juhudi kubwa za vikosi vya uokoaji, zoezi la kuudhibiti moto huo lilikuwa gumu, hasa kutokana na teknolojia hafifu iliyokuwa inatumika miaka hiyo. Moto ukazidi kusambaa kwa kasi kubwa na kuendelea kuteketeza kila kitu kilichopitiwa, siku ya kwanza ikapita, ikaja ya pili na ya tatu huku moto ukizidi kukolea siku baada ya siku.
Kutokana na mabadiliko ya uelekeo wa upepo, hakuna sehemu au mtaa uliosalimika kuteketea, ukaendelea kuwaka mpaka siku ya nne, Jumatano ya Septemba 5, moto huo ulipoanza kupungua wenyewe baada ya kuwa umeteketeza karibu kila kitu kwenye jiji hilo. Baadaye ulizima wenyewe.

Tathmini ya haraka ilionesha kuwa nyumba zaidi ya 70,000 ziliteketea na kusababisha zaidi ya asilimia tisini ya wakazi wa jiji hilo kukosa sehemu za kuishi. Idadi ya watu waliofariki kwenye tukio hilo, mpaka leo haifahamiki lakini inaelezwa kuwa maelfu ya watu waliteketea kabisa mpaka mifupa kutokana na ukali wa moto huo ambao uliweza hata kuyeyusha baadhi ya vyuma.

Inaelezwa kuwa joto la moto huo lilifikia nyuzijoto 1700, kiwango kinachoweza kuyeyusha mpaka mifupa ya binadamu, achilia mbali vyuma na vifaa vingine. Baadhi ya vifaa, vikiwemo vyuma vilivyoyeyuka upande, vimehifadhiwa kwenye Jumba la Makumbusho, London Museum mpaka leo.

Kutokana na ukubwa wa tukio hilo, moto huo ulipewa jina la London Great Fire na inaelezwa kuwa tangu kipindi hicho, hakujawahi kutokea tukio jingine baya la moto kama hilo duniani

Leave A Reply