Mourinho Amsifu Smalling Akishinda

KOCHA wa AS Roma, Jose Mourinho, amesema kuwa ameridhishwa na kiwango cha staa wake Chris Smalling.

Smalling alionyesha kiwango cha juu wakati Roma ilipopata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Zorya Luhansk kwenye michuano mipya ya Europa Conference.

 

Mourinho amesema limekuwa jambo zuri kumuona staa wake huyo akifunga bao na pia akitengeneza nafasi nyingine ya bao.

Mabao mengine ya Roma kwenye mchezo huo yalifungwa na Stephan El Shaarawy na Tammy Abraham.

 

“Ni jambo zuri kumuona akionyesha kiwango cha hali ya juu, kwangu huyu ni mchezaji muhimu sana na naamini kuwa huko mbele anaweza kufanya vizuri zaidi, ni mchezaji mahiri na amekuwa akijituma sana,” alisema Mourinho.

 

Ushindi huo umewafanya Roma wawe hawajafungwa mchezo hata mmoja kwenye michuano hiyo msimu huu katika hatua ya makundi baada ya mchezo wa kwanza kuwafunga CSKA Sofia mabao 5-1.

ROMA, Italia


Toa comment