Kocha Mkuu wa Manchester United, Jose Mourinho amewasili nyumbani kwao Ureno tayari kwa mazishi ya baba yake mzazi mzee Jose Manuel Mourinho Felix.
Jose Manuel Mourinho Felix, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79 baada ya kuugua muda mrefu.
Mazishi yake yanatarajiwa kufanyika leo Mini Setubal na tayari ndugu na jamaa wa familia hiyo wako mjini hapo.
Felix alikuwa mwanasoka na aliwahi kucheza Timu ya Taifa ya Ureno akiwa kipa.
Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.