The House of Favourite Newspapers

Mourinho Azidi Kukomaa na Sanchez Mpaka Kieleweke

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amewasili katika uwanja wa Old Trafford siku ya Jumatano asubuhi huku ikiwa timu hiyo inakaribia kumsajili Alexis Sanchez.

Mourinho amewasili katika maeneo ya mazoezi ya Aon Training Complex wakati mazungumzo na Arsenal yakiendelea ya dau la paundi milioni 35 kunasa saini ya mchezaji wa kimataifa wa Chile, Sanchez.

Baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo wameonekana kuwasili makao makuu ya timu hiyo akiwemo Martial,ambaye alikuwa wakwanza kufunga bao siku ya Jumatatu usiku dhidi ya Stoke na kuchomoza na ushindi wa mabao 3-0.

Marcus Rashford, Juan Mata, Scott McTominay, Daley Blind na Sergio Romero piia wameonekana kuwasili akiwemo na Mcameron, Borthwick-Jackson ambaye amerejea kutoka kwa mkopo Leeds United.

Comments are closed.