Mourinho: Carrick Ameniita Man United

Mourinho:

K OCHA wa Tottenham Hotspur, Jose Mourinho amesema kuwa mtu pekee aliyemwalika kwenye Dimba la Old Trafford ni Michael Carrick.

 

Mourinho kabla hajawa kocha wa Spurs alikuwa kocha mkuu wa Man United lakini akatimuliwa msimu uliopita.

 

Jumatano ijayo, Spurs watakwenda kwenye Dimba la Old Trafford kwa ajili ya kuvaana na Man United ambayo Carrick ni kocha wake msaidizi.

 

Mourinho amesema kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Man United amekuwa akimshukuru kwa muda mrefu kutokana na kuwa yeye ndiye aliyemuingiza kwenye ukocha na amemkaribisha Old Trafford.

 

“Nimekuwa nikipata shukrani nyingi sana kutoka kwa Carrick, nafikiri hadi sasa ndiyo mtu pekee aliyenikaribisha Old Trafford kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu England,” alisema Mourinho.

 

Hata hivyo, inaelezwa kuwa Mourinho atakutana na mashabiki mchanganyiko kwa kuwa wengine watamzomea na wengine watamshangilia kwenye mchezo. Mourinho ameshinda mechi zote ambazo ameiongoza Spurs hadi sasa.
Toa comment