Makala: Imelda Mtema, Gazeti la Risasi Jumamosi, Toleo la Desemba 31, 2016
MPAKA Home inafunga mwaka leo. Inafunga na Mtangazaji na Mtayarishaji wa Kipindi cha Sports Extra cha Clouds TV, Jacob Mbuya. Yeye anaishi maeneo ya Kimara Mwisho jijini Dar. Ndani ya nyumba hiyo aliyopanga, anaishi yeye na mchumba wake ambaye kwa sasa amerudi kwao Kitunda jijini Dar kwa muda kula sikukuu.
Kwa wafuatiliaji wa Clouds TV, Mbuya wanamtazama kupitia kwenye habari za michezo kila siku kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, saa 1:30 hadi 2:00 usiku na Kipindi cha 360 (Alhamisi saa 3:00 asubuhi, kipengele cha michezo).
Mpaka Home imezungumza naye mengi hapa chini. Karibu:
KWA NINI MKEWE KAONDOKA?
“Si unajua tena ndiyo kwanza ametoka kujifungua, bado anapewa mawili matatu na mama mkwe. Hivyo anakuja anakaa kidogo, anarudi tena kwa mama.
RATIBA YAKE IKOJE NYUMBANI?
“Mimi kwa kweli si mtu wa kurudi nyumbani mapema, napenda kutazama mechi mbalimbali za ulimwenguni hivyo hapa narudi masaa machache sana kulala.
HUWA ANATUMIA KILEVI?
“Napiga kilevi ndiyo hususan wikiendi lakini katikati ya wiki mara nyingi huwa situmii. Mwili wangu nautengeneza ninavyotaka na ndiyo maana unaona sinenepi wala sikondi.
USAFI WA NYUMBA
“Huwa nafanya mimi au wakati mwingine anafanya mwenzangu. Sisi tunaishi kama marafiki, tunasaidiana hata kwenye majukumu ya usafi kama hivi unavyoona leo nafagia nyumba nzima.
RATIBA YAKE YA MAZOEZI
“Huwa kila siku hata niwe nimechelewa vipi kulala lakini lazima niamke saa kumi na moja alfajiri, naenda gym kisha naingia uwanjani kupasha kidogo ndiyo narudi nyumbani. Nikirudi, mara nyingi huwa baada ya kuoga, naanza kula matunda kisha baadaye natimka zangu kazini.
HANYWI CHAI?
“Daah mara nyingi huwa nakunywa kawaha ofisini kupasha tumbo moto, baada ya hapo nitakula tena mchana iwe ni wali samaki, chipsi au kitu kingine.
MPANGO WAKE NA SHEMEJI
“Si kwamba nimezaa naye tu ndiyo mipango imeishia hapo, hapana. Namshukuru Mungu nimeshaianza safari ya kuelekea kwenye ndoa. Nishamchumbia hivyo Mungu akipenda mwakani, tutairasimisha ndoa.
SARE YA KAZINI IKOJE?
“Mimi muonekano wangu nyumbani mara nyingi ni wa T-Shirt na jinzi lakini huwa nabeba suti zangu kwenye gari kwa ajili ya kutangazia si unajua huwezi kuwa na muonekano wa kiujana kwenye runinga!
NDOTO ZAKE
“Navutiwa sana na Kituo cha Voice of America (VOA). Ndoto zangu siku moja ni kufanya kazi huko.
KUPIKA VEPEE?
“Kwa kweli mimi si fundi sana katike eneo hilo na mwenzangu anajua. Mfano wali sijui kupika kabisa. Kuna baadhi ya vitu ambavyo najua kama chai, maini na mchemsho wa samaki.
Vingine vyote huwa naviona tu kwa mwenzangu vikiwa vishaiva. Muda wenyewe si unajua, ni nadra sana kunikuta nyumbani.
YUKO PEACE NA MAJIRANI?
“Yeah! Jirani wangu wa kwanza ni mama mwenye nyumba yangu. Naye anaishi hapa jirani na mimi, tunaishi vizuri na ni shabiki wangu pia. Anafuatilia sana vipindi vyangu vya michezo kwani naye anapenda michezo.
WIKIENDI HUWA INAKUWAJE?
“Mara nyingi huwa Jumamosi nawahi sana kurudi nyumbani maana huwa ratiba yangu ya Jumapili inakuwa ndefu kidogo. Naanzia kanisani misa ya pili (Kanisa Katoliki, Mashahidi wa Uganda-Magomeni), nikirudi nalala kidogo kisha nikiamka napiga msosi, naelekea Magomeni kucheza mechi maana mimi naichezea Timu ya Migration ya Magomeni ambapo kila Jumapili huwa tunakuwa na mechi.
SHUKRANI KWA MPAKA HOME
“Niwashukuru sana kwa kuja kunitembelea, karibuni tena siku nyingine.”
Gazeti la Risasi Jumamosi, Toleo la Desemba 31, 2016
BELLE9 KIBOKO, CHEKI ALIVYOIMBA NYIMBO YAKE MPYA YA GIVE IT TO ME, SHOW YA FUNGA MWAKA ESCAPE ONE
Comments are closed.