The House of Favourite Newspapers

MPAKA HOME: Makabila Amwanika Mpenzi Wake

0


NA IMELDA MTEMA | RISASI JUMAMOSI | MPAKA HOME

MAMBO vipi mpenzi msomaji wangu wa safu hii murua ya Mpaka Home, kama ilivyo kawaida ya kila wiki tunakuletea maisha halisi ya kila siku ya mastaa mbalimbali.

Leo tunaye kijana mdogo ambaye hivi karibuni ameweza kujizolea umaarufu mkubwa sana kutokana na wimbo wake wa Hujaulamba, si mwingine ni Dulla Makabila anayeishi Sinza-Mori, jijini Dar akiwa bado kijana bachela, ungana nami chini uweze kujua mengi zaidi.

Dulla Makabila akichambua mchele

MPAKA HOME: Habari, nilitegemea hapa kwako nitamkuta wifi , mbona kama upo peke yako?

DULLA: Hakuna wifi bado kabisa bisa maana itan- i chukua muda kidogo.

MPAKA HOME: Nilijua ishu za jiko huwezi kuwanazo kwa vile ni mwanaume na pia staa, ni kweli au si siyo kweli?

DULLA: Mimi suala la jikoni nalipenda nafi kiri pia ni kwa sababu   da sana kula kitu ambacho kimepikwa vile ninavyotaka.

MPAKA HOME: Ni chakula gani unapendelea kula hata kukipika mwenyewe?

 

DULLA: Kupika wali na nyama.

MPAKA HOME: Ukiacha wali ni chakula gani kingine unapendelea kula?

DULLA: Ugali wa dona kwa samaki wa kukaangwa, kwa mfano nikila mlo huo mapema, kutwa nzima nashindia kunywa maji tu hadi jioni.

MPAKA HOME: Bado hujaoa lakini vipi kuhusu mpenzi, unaye?

DULLA: Ninaye ambaye naye ni staa mkubwa tu.

Husna Sajent katika pozi

MPAKA HOME: Mashabiki wako wangependa sana kumjua, tafadhali funguka.
DULLA: Ni Sajent, yaani huyu mwanamke nampenda sana.

MPAKA HOME: Sajent huyuhuyu mama Carina?

DULLA: Ndiyo huyohuyo ila tu sitaki kuzungumza mengi zaidi ila ndiye mtarajiwa wa baadaye MPAKAHOME: Unapokuwa na hasira cha kwanza unafanya nini?

DULLA: Mara nyingi napenda kuondoka eneo la tukio ili kuepusha shari.

 

MPAKA HOME: Mara ya mwisho kula chakula kwa mama ntilie ni lini?

DULLA: Yaani mpaka sasa nakula tena napendaga ukoko wa wali, siwezi kuacha hiyo hata kama ni staa. MPAKA HOME: Mara ngapi umeshawahi kupiga usingizi sebuleni?

DULLA: Yaani mimi sasa tabia yangu ni nyingine, napenda kulala kwenye korido ndiyo mchezo wangu, kitandani huwa sipendi.

 

MPAKA HOME: Kitu gani kimewahi kukuumiza sana maishani?

DULLA: Niliponyan’ganywa maiki na kuzomewa kwa kuonekana sijui kuimba nilipopanda jukwaani kwa mara ya kwanza.

MPAKA HOME: Nakushukuru kwa ushirikiano.

DULLA: Asante sana.

 

Prof Jay: Bajeti Wizara Ya Ujenzi Haitekelezeki

Leave A Reply