The House of Favourite Newspapers

Mpambano wa Nichane Nikuchane, R.O.M.A Vs Darassa Gumzo ‘Vichwa Kuwaka Moto’, Dar Live

darassa-vs-romaZimesalia siku 15 tu kufikia Mkesha wa Mwaka Mpya ambapo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar, wakali wawili ambao hawashikiki kunako Muziki wa Hip Hop Bongo, Shariff Thabeet ‘Darassa’ na Ibrahim Musa ‘R.O.M.A Mkatoliki’ wameanza kuonesha kupaniana katika mpambao wao wa kimuziki unaokwenda kwa jina la Nichane Nikuchane ambao ni gumzo kila kona kwa sasa.

Wawili hao wanatarajiwa kukutana kwa mara ya kwanza katika historia ya muziki huo ndani ya jukwaa la Dar Live katika mpambano huo mkali  wa ‘rap battle’ unaotarajiwa kushuhudiwa na mamia ya watu.

darassa-4Darassa

Akizungumzia usiku huo ambao unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa burudani hususan wapenda Hip Hop Bongo, Darassa aliwataka mashabiki wake wajitokeze kwa wingi kwani siku hiyo ataonesha umwamba.

“Sina maneno ya kwenye kanga, ngozi yangu inatosha kujigamba kama nilivyoimba kwenye Muziki. Kikubwa tukutane kwenye Usiku wa Nichane Nikuchane Dar Live.

“Nimejipanga vya kutosha, siku zote nikiwa jukwaani sijawahi kumuangusha shabiki wangu hivyo hii si ya kukosa,” alijitapa Darassa anayetikisa na Ngoma ya Muziki.

romaR.O.M.A

Kwa upande wa R.O.M.A Mkatoliki alisema, usiku huo atafanya shoo ya kitofauti kutokana na mpambano hivyo kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia.

“Huwa siongei sana ila CV yangu inatosha kujieleza. Dar Live ni uwanja wa nyumbani na pointi tatu ni muhimu kuchukua siku hiyo.

“Mara ya mwisho kupiga shoo hapo ilikuwa miaka miwili iliyopita tena nikiwa na ngoma chache lakini sasa hivi nina ngoma mpya kibao ambazo nitapambania nazo kama Viva Roma Viva, Una Akili Wewe, Mmeniroga remix na Kaa Tayari,” alisema R.O.MA.

rap-battleMkwanja sasa!

Akizungumza na Tovuti ya Global Publishers, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo aliweka wazi kuwa wanataka kila shabiki wa burudani aingie hivyo kiingilio ni sawa na bure.

“Tungeweza kuweka kiingilio kiwe bure ili kila mmoja ashuhudie mpambano huu ambao haujawahi kutokea. Tumeamua kuwa kiingilio kiwe shilingi 5,000 tu na kwa watu 3000 wa kwanza watapata ofa ya kupiga picha na mastaa hao,” alisema Mbizo.

Hawa pia watakuwepo

Mbizo aliongeza kuwa, shoo inatarajiwa kuanza saa saba mchana mpaka majogoo.

“Tutakuwa na wasanii wengi watakaosindikiza mpambano huu likiwemo kundi lisilo na mpinzani Bongo katika Muziki wa Taarab la Jahazi Modern. Tutakuwa na mkongwe wa Bongo Fleva, Sir Juma Nature, H-Mbizo, Makhirikhiri kutoka Tanzania, MC Darada, ID Classic na wengine wengi,” alimaliza Mbizo.

Darassa ft Ben Pol – Muziki ( Official Music Video )

Roma featuring Jos Mtambo & Darasa – KAA TAYARI (OFFICIAL VIDEO)

Comments are closed.