The House of Favourite Newspapers

Mpango Kabambe Wa Usalama Barabarani Wazinduliwa Na Jeshi La Polisi Kwa Kushirikiana Na TBL

0
Mwanasheria na Mratibu wa mafunzo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, SSP Deus Sokoni (kushoto) akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.

Dar es Salaam, 31 Oktoba 2023 — Tanzania Breweries Ltd. (TBL), Kampuni tanzu ya AB InBev, inafuraha kutangaza kuanza kwa mfululizo wa mafunzo ya kina kwa Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani.

Programu hii wa mafunzo itawatambulisha maofisa hao kwenye mapinduzi ya programu ya simu ya mkononi (Mobile App) iliyoandaliwa kupitia jitihada za ushirikiano kati ya Kikosi cha Usalama Barabarani na TBL.

Mkuu wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kipolisi Kinondoni SSP, Solomon Mwangamilo akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Programu hii bunifu imewekwa ili kuunda upya mazingira ya ukusanyaji, uchanganuzi na utoaji wa taarifa na takwimu za Askari wa Usalama barabarani nchini.

Programu mpya ya simu ya mkononi iliyotengenezwa itachukua jukumu muhimu katika kurahisisha ukusanyaji wa taarifa za Askari wa usalama barabarani, kwa kuruhusu maafisa kuandika na kupakia taarifa za matukio moja kwa moja kwenye seva salama. Hii itawezesha Jeshi kuondokana na mifumo ya sasa, ambapo taarifa hukusanywa katika vituo vya polisi kimoja kimoja, na hatimaye kukusanywa kwa wilaya, mkoa, na hatimaye kitaifa.

Askari wa usalama barabarani wakipata mafunzo kutoka kwa mkufunzi (aliyevaa kiakisi mwanga).

Manufaa ya mfumo huu mpya ni mengi kwa Jeshi la Polisi Tanzania, watathimini mipango ya barabara, makampuni ya bima na wadau wengine. Kwa ufikiaji wa data ya wakati halisi, mipango na usimamizi wa usalama barabarani utakuwa sahihi na mzuri zaidi. Zaidi ya hayo, madereva pia watafaidika kutokana na kuharakisha kwa madai ya bima, kupunguza muda na utata unaohusishwa na taratibu hizo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Usambazaji wa TBL, Nancy Riwa alisema ni fahari na heshima kubwa kwa TBL kuwa sehemu ya mpango huo muhimu. Alitoa shukrani za kampuni hiyo kwa ushirikiano na msaada walioupata kutoka kwa Jeshi la Polisi Tanzania wakati wote wa utayarishaji wa mfumo huu mpya.

Mkurugenzi wa Usambazaji wa TBL, Nancy Riwa (kulia) akimkabidhi simu hizo Mkuu wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kipolisi Kinondoni SSP, Solomon Mwangamilo (kushoto). Anayeshuhudia katikati ni  Mwanasheria na Mratibu wa mafunzo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, SSP Deus Sokoni

TBL inatambua mchango na busara uliotolewa na Jeshi la Polisi katika kuandaa muundo wa program hii. Mpango huu ni mwendelezo wa ushiriki wa muda mrefu wa TBL katika kusaidia usalama barabarani nchini, na kusisitiza dhamira ya kudumu ya kampuni hiyo kusaidia Polisi wa Usalama Barabarani na wadau wengine.

Katika taarifa yake, Riwa alisema, “Tanzania Breweries Ltd. inajivunia kupewa heshima ya kuwa sehemu ya mpango huu muhimu sana. Tunashukuru kwa ushirikiano na msaada wa Jeshi la Polisi la Tanzania kwa kufanya kazi nasi kuunda hii programu mpya.

Tunatambua mchango wao wa busara katika uundaji wa program. Huu ni mwendelezo wa historia ndefu ya ushiriki wetu katika usalama barabarani nchini, na tunapenda kusisitiza tena dhamira yetu ya kuendelea kusaidia Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na wadau wengine kuhakikisha kwamba tunajenga mifumo imara na madhubuti ya usalama barabarani katika nchi hii ili kupunguza ajali na natumaini siku moja kukomesha vifo vitokanavyo na ajali barabarani zinavyoweza kuzuilika.”

Mwanasheria na Mratibu wa mafunzo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, SSP Deus Sokoni alieleza kushukuru kwa Jeshi la Polisi Tanzania kwa msaada linalopata na jukumu lililopo katika kuwawezesha kutekeleza majukumu yao.

Akifungua mafunzo hayo alisema, “Ukusanyaji wa takwimu sahihi na kwa wakati una umuhimu mkubwa wakati wa kupanga, kufuatilia na kutathmini afua za usalama barabarani na pia kwa ajili ya utendaji kazi wa wadau mbalimbali.

Tanzania ina Sera ya Usalama Barabarani iliyoanzishwa mwaka 2009 ambayo inaweka wajibu kwa wadau wote. TBL inatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya ukusanyaji sahihi na kwa wakati wa data utasaidia pakubwa utekelezaji wa sera hii.”
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkuu wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kipolisi Kinondoni SSP, Solomon Mwangamilo alisema, “Napenda kuwashukuru TBL kwa kupaza sauti zao na kushirikiana na Jeshi la Polisi, hii itaimarisha sana usimamizi wa sheria kwa watumiaji wote wa barabara na kuleta utendaji hadi kiwango cha dijitali.

Kama Jeshi la Polisi tunatakiwa kuingia haraka katika zama za kidijitali. Utumiaji wa kifaa hiki ndio hasa tunachohitaji ili kupata taarifa kwa wakati na hivyo ni lazima tuvitunze.”
Mpango huu wa kihistoria sio tu unasisitiza dhamira ya TBL kwa usalama barabarani nchini Tanzania bali pia nia yake ya kuendeleza ubunifu na teknolojia kwa ajili ya kuboresha taifa.

Mpango wa mafunzo hayo utawapatia Maafisa wa Usalama Barabarani maarifa na zana wanazohitaji ili kuleta athari chanya katika kusimamia usalama barabarani nchini Tanzania, na hatimaye kufanya kazi kwa lengo la kupunguza matukio ya ajali za barabarani zinazoweza kuzuilika.

Kuhusu Tanzania Breweries Ltd. (TBL)
Tanzania Breweries Ltd. (TBL) ni kampuni ya vinywaji inayoongoza nchini Tanzania na kampuni tanzu ya AB InBev. Kwa dhamira thabiti ya uwajibikaji wa shirika kwa jamii, TBL inashiriki kikamilifu katika mipango inayochangia usalama barabarani, mazingira endelevu, na maendeleo ya jamii nchini.

Leave A Reply