The House of Favourite Newspapers

MPENZI WA BABY J AMCHANA ESMA!

MAPENZI bwana, kweli ni upepo wa Kisulisuli! Mzazi mwenziye na mwanamuziki maarufu visiwani Zanzibar, Jamila Abdalah ‘Baby J’, Abood amemtaka Esma aache kumchafua kwenye mitandao ya kijamii na kumuambia kuwa ameamua kumrudia mzazi mwenziye na kumwambia kuwa asingeweza kumuoa kwa vyovyote vile.

Akizungumza na Amani, Abood alisema kuwa ni kweli alipotea njia na kwenda mahali sipo (kwa Esma) kutokana na tamaa na kumsaliti mzazi mwenziye, lakini kwa sasa amesharudi. Hivyo Esma aache kumchafua kwa watu hususan katika mitandao ya kijamii.

“Mimi ningemuomba tu Esma aache kunichafua kabisa, nimeshaamua kurudi kwa mama mtoto wangu hivyo aniache kwa sababu na mimi nina mengi sana ya kwake, tuheshimiane,” alisema Abood. Jamaa huyo alifunguka hayo kufuatia kusambaa kwa sauti mitandaoni inayosemekana ni ya Esma akimsema vibaya Abood.

Stori: Imelda Mtema

Comments are closed.