The House of Favourite Newspapers

Mpenzi wa Chris Brown aonekana tena na Depay Jijini Manchester

0

2CDED5CD00000578-0-image-a-54_1443468846612

2CDECF7100000578-0-image-a-55_1443469034106

2CDED0F800000578-3252567-image-a-5_1443471119549

Mpenzi wa zamani wa msanii Cris Brown wa Marekani, Karrueche Tran akiwa na  mchezaji wa Manchester United, Memphis Depay wakiwa mitaani katika jiji la Manchester.

KIUNGO  mwenye kasi wa Manchester United, Memphis Depay sasa hawezi kusema tena ni urafiki tu kati yake na mrembo Karrueche Tran.

Depay na Karrueche, 27, wameonekana mitaani katika jiji la Manchester wakifanya manunuzi, huku kukiwa na ‘mtembeo’ unaoashiria kuficha kitu na si marafiki pekee.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 aliwahi kuonekana na mpenzi huyo wa zamani wa msanii Cris Brown wa Marekani, lakini ikaelezwa ni ‘marafiki tu’.

Hata hivyo, baadaye kukawa na taarifa kwamba wana uhusiano wa kimapenzi. Licha ya kuficha, lakini sasa mambo yanaonyesha kwamba lazima watakuwa pamoja.

Pamoja na kuonekana mtaani, lakini usiku walionekana wakiwa katika klabu moja wakila raha.

Mastaa wengi wamekuwa si wepesi kuanika uhusiano walionao hadi pale unapokolea na hii huonekana wengi kuwa na hifu hadi hapo mambo watakapokuwa na uhakika nayo, ndiyo huwa tayari kuweka mambo hadharani.

Leave A Reply