Mpenzi wa Kanye Apata Dili Nono

Mpenzi mpya wa Kanye West, Julia Fox amelamba dili kubwa Hollywood la kuigiza katika filamu ya msanii nguli na mashuhuri wa Pop Duniani MADONNA. Julia Fox ataigiza kama rafiki wa muda mrefu wa Madonna anae fahamika kama Debi Mazar.
Radar wana repoti kuwa tayari Julia Fox amekutana na Madonna na team yake kwaajili ya kuongelea husika hio huku pakiwa na maswali mengi kuhusu Julia Fox kupata mchongo huo sababu amekuwa hot sana duniani baada ya kuanzisha mahusiano na Kanye West.

