The House of Favourite Newspapers

MPENZI WA NAI AKERWA NA UGOMVI

Nai Kisa

MUUZA sura kwenye video za wanamuziki Bongo, Nai Kisa amefunguka kuwa mpenzi wake ambaye ni mwanamuziki wa Hip Hop, Moni Central Zone amekuwa akikerwa na ugomvi wake na wasanii wenzake maana ni kitu ambacho hakipendi.

 

Akichezesha taya na Mikito Nusunusu, Nai alisema huwa analazimisha tu kuwajibu wanaomsema vibaya mitandaoni, lakini ukweli ni kwamba mpenzi wake huyo hapendi na amekuwa akimkataza mambo hayo mara kwa mara.

Mwanamuziki wa Hip Hop, Moni Central Zone

“Katika vitu ambavyo mpenzi wangu Moni hapendi ni mimi kuwa na ugomvi na wenzangu hasa mitandaoni. Huwa anakereka sana na mara nyingi amekuwa akiniambia nikae kimya, lakini kuna wakati nashindwa kuvumilia matusi na maneno mabaya ambayo nakuwa naambiwa na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo yangu, hivyo najikuta nimewajibu ili na mimi nafsi yangu iridhike,’’ alisema Nai.

STORI: Memorise Richard

Comments are closed.