The House of Favourite Newspapers

Mpigania Uhuru Aliyekuwa na Nelson Mandela Sauzi, Ahmed Kathrada Afariki Dunia


Kiongozi mwanaharakati aliyeshiriki katika kupigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, Ahmed Kathrada amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87.

Kathrada alifariki dunia akiwa katika hospitali moja mjini Johannesburg baada ya kuugua kwa muda mfupi, kufuatia upasuaji aliofanyiwa kwenye ubongo wake.

Pamoja na Nelson Mandela, Kathrada alikuwa miongoni mwa wanaharakati wanane wa African National Congress waliohukumiwa kufungwa jela maisha mwaka 1964.

Ahmed Kathrada akiwa na Mandela

Walipatikana na hatia ya kujaribu kupindua serikali ya ubaguzi wa rangi, ambapo Kathrada alihukumiwa kwenda jela miaka 26, 18 kati ya miaka hiyo akiwa katika gereza hatari la Robben Island na kuachiliwa huru mwaka 1989.

Rais Mandela baadaye alimshawishi kujiunga na serikali.

Ahmed Kathrada aliondoka bungeni 1999, lakini aliendelea kushiriki katika siasa nchini humo.

Alikosoa mwelekeo wa chama cha ANC hivi majuzi na kumtaka Rais Jacob Zuma kujiuzulu.

Comments are closed.