The House of Favourite Newspapers

Mpoto: Afungua kampuni na kuwaweka warembo tu

0

TX4A1433-1200x930MPENZI msomaji wa simulizi hii tamu na ya kusisimua ya Mrisho Mpoto, wiki iliyopita tuliishia pale alipotoa siri ya kwa nini hapendi kuwaanika watoto na mkewe kwenye vyombo vya habari hususan kwenye mitandao. Pia Mrisho alizungumzia siri ya kwa nini alikataa kugombea ubunge wa Mbagala ingawa aliombwa na Diwani wa Mbagala, Yusuf Manji.Songa nayo…

“Maisha yangu na nguvu zangu zote nimeamua kuzielekezea kwenye kusaidia jamii, kusaidia watu hususan vijana ambao ni taifa la kesho, vijana ambao ukiongelea kwa sasa ni tegemeo katika kufanikisha kila kitu.

“Kwa kuwa nilikuwa sihitaji kujiingiza kwenye siasa kabisa, niliamua nijijengee njia yangu ya kuwasaidia hawa vijana ninaowaongelea hata siku moja niwe role model wao ambapo nikafungua Shirika Lisilo la Kiserikali (NGO’s) linalojulikana kwa jina la Mpoto Foundation lenye lengo la kuwasaidia vijana wale waliokata tamaa na maisha.”

Safi sana Mrisho na hongera kwa hatua uliyoamua kuichukua katika kusaidia vijana. Embu fafanua vizuri hapo kwenye hiyo faundation yako.

“Ahaa, Ni kwamba vijana wengi nchini wamekumbwa na kasumba ya kutojua kusoma yaani kupitia darasani, vijana wengi ni chokoraa, vijana wengi wanao uwezo wa kulima lakini bado wanashindwa kujituma na kudai hakuna ajira nchini.

“Nimeamua kufuta ile dhana ya vijana ni wengi nchini kuliko uzalishaji wa chakula. Nikaamua niwatengee shamba la ekari 35 na huko watakaa kwa muda mrefu nikiwapika jinsi ya kupambana na maisha sambamba na kujifunza kuimba ili wafike nilipo hapa leo hii.

“Bado sijaanza rasmi kuwaweka kijijini katika mashamba lakini nilitoa nafasi kwa vijana hamsini ambao watakuwa tayari kuwa katika kijiji hicho chenye ekari 35 na kwa kwenye usaili tu walijitokeza vijana zaidi ya 2,000 hawana ajira na wanahitaji kujikita vijijini, vijana hao walikuwa wapo tayari kufanya kazi na mimi bila hata ya kulipwa.”
Mbali na hiyo foundation, kuna kingine kinachowasaidia vijana?

“Ndiyo, niliamua pia niwaangalie na vijana wa kike katika kuwasaidia kujikwamua na ajira ambapo nimefungua Kampuni ya Interna-tional Market (IM) inayodili na kupokea tenda mbalimbali na kuzifanyia kazi. Mfano viwanja na mashamba. Sasa hii IM inaendeshwa na vijana wa kike pekee (warembo) zaidi ya 19 ambao niliwatoa sehemu mbalimbali za starehe kwani niliamini vijana wengi wa kike wanaweza kupatiwa fedha bila maradhi. Vijana hao wa kike leo hii wanaendesha IM bila matatizo na wameweza kujitoa sehemu mbalimbali za starehe walizokuwepo.

“Mbali na hiyo tena nina Mpoto Theatre Gallery ambapo ndani yake kuna kundi la wasanii wa nyimbo za asili, nyimbo ninazozifanya. Kama utaona kwenye matamasha mengi makubwa ninayofanya huambatana na kundi langu.”

Itaendelea wiki ijayo.

JIUNGE NA GLOBAL BRAKING NEWS

GLOBALBREAKINGNEWS100.jpg

Leave A Reply