The House of Favourite Newspapers

Mpoto Asikitishwa na Wanamuziki

0

Na Boniphace Ngumije | UWAZI | SHOW BIZ

MWANAMUZIKI anayefanya vizuri katika gemu la Muziki wa Asili nchini, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ ameonyesha kusikitishwa na wanamuziki wenzake wanaofanya muziki wa aina hiyo kwa kukosa ubunifu, jitihada na maarifa ya kuukuza zaidi ya kuzidi kuudidimiza.

Akipiga stori na Uwazi Showbiz, Mpoto aliongeza kuwa wasanii wengi wa muziki huo wamekata tamaa kutokana na muziki wa asili kupoteza msisimko kama ilivyokuwa zamani, lakini pia aliongeza kuwa wanaotakiwa kuunusuru ni wasanii wao wenyewe.

“Ni kweli Muziki wa Asili umekosa msisimko, wanamuziki inabidi waamke na kuwa wabunifu ili kurejesha heshima ya muziki wa asili nchini,” alisema Mpoto.

Leave A Reply