The House of Favourite Newspapers

Marafiki wadai…Mpoto ni Freemason

0

IMG_0883
Staa wa muziki wa asili na mtunzi wa mashairi Bongo, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ akiwa kwenye jengo la Taasisi ya Freemason lililopo Posta jijini Dar.

BALAA! Staa wa muziki wa asili na mtunzi wa mashairi Bongo, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’, juzi alinaswa na makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kwenye jengo la Taasisi ya Freemason lililopo Posta jijini Dar na kuzua viulizo.

Makamanda wetu walipewa taarifa na mtu wa karibu na eneo hilo kuwa msanii huyo alionekana akirandaranda kwenye jengo hilo pasipo kujua lengo la kwenda mahali hapo ni lipi kama si mfuasi wa taasisi hiyo.

IMG_0886
“Jamani namwona Mpoto hapa getini kwenye jengo la Freemason. Ni muda yupo hapa, amevaa mkanzu mweupe. Sijui na yeye ni mfuasi wa hawa watu. Kama vipi muwahi wenyewe mjionee. Amepaki gari lake hapa,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuunyaka ubuyu huo, mapaparazi wetu walitinga eneo hilo na kumkuta Mjomba huyo akiwa amesimama nje ya gari lake aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T 371 DCE kwenye eneo la kuegeshea magari ya jengo hilo.

IMG_0882
Baada ya muda, staa huyo alitoka aliposimama na kwenda kuingia kwenye jengo hilo huku baadhi ya wananchi wakimtupia macho ya mshangao.

“Jamani huyu Mpoto humo Freemason kumempataje! Au na yeye ni mshirika? Inawezekana hata mafanikio aliyonayo kwa sasa yanatokana na uwepo wake kwenye chama hicho,”alisikika mmoja wa watu hao.

IMG_20150914_140112Hata hivyo, msanii huyo hakuchukua muda mrefu ndani ya mjengo huo akatoka huku akiongea kwa simu na kuelekea kwenye gari lake kisha akatokomea kusikojulikana.

Ilibidi mapaparazi wetu wampigie simu na kumuuliza kuhusu uwepo wake kwenye jengo hilo ili kutatua kitendawili hicho ambapo alijibu:

IMG_20150914_140157“Mh! Nyie mlikuwa kwa wapi? Mmeniona, mmeambiwa? Ni kweli nilikuwepo eneo hilo lakini kuna mgombea ubunge nilikwenda kuonana naye. Anataka nimtungie mashairi ya wimbo. Hayo mengine ya mimi kuwa mshirika wa watu hao siyajui mlikoyatoa.”

IMG_0890Amani: Huyo mgombea ubunge alikuwa ndani ya lile jengo?”

Mpoto: (alikata simu na hakuwa hewani tena).

IMG_20150914_140231Kufuatia mafanikio yake ya kasi, siku za hivi karibuni, baadhi ya marafiki wa msanii huyo wamekuwa wakisema jamaa ni Freemason taasisi ambayo inasimamia kwenye kuisaidia jamii licha ya kudaiwa kuwa na ibada yenye kutia shaka. Hata hivyo, madai hayo yamekuwa yakipingwa na viongozi wake kila siku.

Leave A Reply