Mr Bean aachana na mkewe kisa, kibinti
County Durham, Uingereza
Muigizaji na mchekeshaji maarufu duniani, Rowan Atkinson ‘Mr Bean’ amelazimika kutoa talaka ya haraka kwa mkewe Sunetra Sastry baada ya kugundulika kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na msichana ‘mbichi’ aitwaye Louise Ford.
Mr Bean inadaiwa alianza kutoka na binti huyo takriban miezi 18 iliyopita na inaelezwa kuwa ni sawa na kumbemenda kwani kiumri (haukutajwa umri wake) ni kama mwanaye.
Hata hivyo, alivyobainika kuwa anachepuka, kuua soo akampa talaka mkewe. Mr Bean na Louise waliingia kwenye uhusiano kwa kuunganishwa na kazi kwani hata Louise ni msanii wa filamu za vichekesho.