Mr blue afungukia kuoa mke wa pili

MSANII wa Bongo Fleva, Kheri Sameer Rajab ’Mr Blue’ amesema katika vitu ambavyo hajawahi kujutia ni pamoja na yeye kuoa na ana furaha ya kuwa na mke sahihi ambaye hawezi kumshawishi kuoa mke wa pili. Akizungumzia maisha ya ndoa, Blue alisema anashangaa kuona vijana wengi wanaogopa kuoa kwa kuhofia majukumu lakini kitu ambacho hawakijui ni kwamba mbali na baraka za Mungu lakini pia ndoa ina raha yake.

“Nashukuru nimepata mke sahihi, siwezi kumuolea mke wa pili licha ya kwamba dini yangu inaruhusu, wito wangu ni vijana kuoa, wasihofie majukumu, ndoa ni tamu sana hasa pale unapompata mke sahihi.

“Vijana wanaogopa sana kuoa siku hizi kwa kuhofia majukumu lakini ukweli ni kwamba mtoto wa kiume hutakiwi kuogopa wala kuyakimbia majukumu, ndio maana hata katika vitabu vya dini imeandikwa kwamba wanaume tutakula kwa jasho,” alifunguka Blue.


Loading...

Toa comment