MR. BLUE: KUNA WAKATI SIAMINI KAMA WATOTO NI WANGU

MAMBO vipi mpenzi msomaji wangu, kila siku iitwayo leo lengo langu kubwa ni kukupatia kitu ambacho kitau-konga moyo wako.  Safu hii ni maalum kabisa kwa mastaa mbalimbali Bongo, ambao tayari wamejaaliwa watoto hivyo wanatudadavulia maisha halisi wanayoishi na familia zao.

Leo tunaye staa wa Bongo Fleva, Hery Sameer ‘Mr. Blue’ ambaye anafa-fanua jinsi anavyoishi na watoto wake pamoja na mkewe. Amefunguka mengi ambayo watu hawayajui. Ungana na mimi hapa chini; Wikienda: Umekuwa ni kati ya mastaa wa kuigwa kutokana na kuiweka familia yako mbele, labda nini kinachokufanya kuwa hivyo.

Mr. Blue: Unajua familia yangu nimeichagua mwenyewe na kitu nilichokichagua ni vyema hata mashabiki wangu wakakifahamu, hakuna sababu ya kufichaficha.

Wikienda: Wewe ni baba wa aina gani?

Mr. Blue: Ni baba ninayeipenda sana familia yangu na kujua nini ninachotakiwa kufanya ili watoto na mke wangu wafurahie uwepo wangu hapa duniani.

Wikienda: Unajisikiaje unapokaa na watoto wako?

Mr. Blue: Kwa kweli najisikia vizuri sana na kuna wakati siamini kabisa kama mimi ndiyo baba wa watoto hao kwa sababu unapomuangalia mtoto wako mmoja unajiona wewe kabisa kwa kila kitu anachofanya.

Wikienda: Mara nyingi unapenda kuongozana na watoto wako, nini siri yako?

Mr. Blue: Kwanza napenda sana watoto tangu, hata sijafikiria kama nitakuja kuoa na kubahatika kupata watoto hawa, hivyo nilivyopata watoto furaha ikawa mara dufu.

Wikienda: Tumeona baadhi ya mastaa kabla hata ya kuingia kwenye ndoa tayari wana watoto nje ya ndoa, unazungu-mziaje hilo?

Mr. Blue: Unajua nimelelewa upande mmoja wa mama tu, hivyo sikuwa napata malezi yale ya wazazi wawili. Nilikuwa naona shida yake kwani kama mtoto hupati malezi yanayostahili kutoka kwa wazazi, ndio maana sijataka kabisa mimi kuwa hivyo.

Wikienda: Unajisikiaje unapokuwa mbali na watoto wako?

Mr. Blue: Unajua ninapotoka nyumbani kwenda mbali, najua wazi nafanya hivyo kwa sababu ya kuwa-tafutia wao lakini ninapokaa huko siku mbili yaani nachanga-nyikiwa kwa jinsi ninav-yowa-kumbuka.

Wiki-enda: Una mpango wa kuongeza watoto wengine?

Mr. Blue: Kabisa maana kwa upande wa baba yangu niko peke yangu na hata kwa mama yangu tupo wachache hivyo ninahitaji tuwe wengi. Kingine napenda sana watoto.

Wikienda: Kuna mtoto wako yeyote anayefuata nyayo zako?

Mr. Blue: Yupo yule wa kiume namuona anaimbaimba lakini nadhani anafanya hivyo kwa sababu anamuona baba anaimba. Ila ana vitu vingivingi, mwingine bado sijajua ila siwapangii kitu cha kufanya maishani mwao.

Wikienda: Asante sana kwa ushirikiano wako.

Mr. Blue: Karibu tena.


Loading...

Toa comment