Mr Blue: Nitamtegemea Chid Benz Hata Iweje

MKALI wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Khery Sameer almaarufu kama Mr.Blue amefunguka kuwa atamtegemea rapa mwenzake Chidi Benz kwenye shoo hata kama akiwa hayupo.

 

Akizungumza kwenye mahojiano na kipindi cha Big 20 Count Down kinachoruka kila Jumapili kupitia +255 Global Radio, Blue alisema kuwa Chidi Benz akiwa jukwaani huwa na msaada mkubwa sana kwani hunyanyua umati wa watu hata kama shoo iko mwishoni.

“Aaah mimi kwenye shoo hakuna mtu namheshimu na nitaendelea kumtegemea mpaka kesho kama Chidi Benz kwani anaweza kuinua raia hata kama shoo iko mwishoni na hata akiwa hajaalikwa ndiyo maana nasema huyo siyo mtu wa kawaida mzee,” alisema Mr. Blue


Loading...

Toa comment