Mr. Championi alivyoteka wasomaji wake Dar
Mr .Championi akimpatia zawadi msomaji wa Gazeti la Championi Jumamosi aliyekutwa akiwa na rafiki yake eneo la Kimara Temboni wakilisoma gazeti hilo.
Mmoja wa wasomaji hao wa Gazeti la Championi akionesha furaha yake mara baada ya kumwona Mr.Championi.
Mdau wa Gazeti la Championi aliyejitambulisha kwa jina la Adinan mkazi wa Mbezi-Mwisho akimwonesha Mr. Championi baadhi ya kurasa anazopendelea kuzisoma.
Msomaji huyo wa Gazeti la Championi akirudishiwa pesa yake aliyonunulia gazeti mara baada ya kukutwa nalo.
Mwanadada ambaye ni mpenzi wa kusoma Gazeti la Championi akipozi na Mr.Championi mara baada ya kupokea zawadi yake eneo la Mbezi-Maramba Mawili.
Mdau wa kusoma Gazeti la Championi akirudishiwa pesa yake na Mr.Championi mara baada ya kushuka katika gari lake eneo la Mbezi-Kifuru.
KAMA kawaida yake Mr.Championi kuwajali wasomaji wake, leo tena ametembelea viunga mbalimbali vya maeneo ya Kimara-Temboni, Mbezi kwa Msuguri, Mbezi Mwisho, Mbezi Maramba Mawili pamoja na Kifuru-Kinyerezi jijini Dar es Salaam na kuwateka wasomaji wake kwa kugawa zawadi mbalimbali sambamba na kuwarudisha pesa yao waliyonununulia Gazeti la Championi.
Wakati wa utoaji zawadi hizo, Mr. Championi aliambatana na ofisa usambazaji wa Global Publishers, Yohana Mkanda, ambaye alikuwa akipokea maoni mbalimbali yanayohusu Magazeti ya Championi pindi alipokuwa akigawa zawadi.
Aidha, Mkanda amewaahidi wasomaji wa Gazeti la Championi kuendelea kulisoma kila linapotoka yaani Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi kwani kila atakayekutwa na Mr.Championi akisoma gazeti hilo atajipatia zawadi papohapo.
NA DENIS MTIMA/GPL