Mr. Chuz aachana na filamu

chuzi3 (1)Gladness Mallya

MKONGWE kwenye gemu la filamu Bongo, Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuz’ ameamua kuachana na filamu kwa kile alichodai kwamba hazilipi.

Akichonga na paparazi wetu, Mr. Chuz alisema soko la filamu limeshuka na wasambazaji wanasuasua, jambo linalofanya maisha ya wasanii kuwa magumu, hivyo ameamua kuachana nayo na kujikita katika kutengeneza tamthiliya ambazo zinarushwa na Runinga ya Africa Magic.

“Nimeachana na filamu maana hazinilipi, soko lenyewe halieleweki, nimeamua kutengeneza tamthiliya ambapo naona kiukweli zinanilipa sana, nakuwa bize muda wote,” alisema Mr. Chuz.

Loading...

Toa comment