The House of Favourite Newspapers

Mr Flavour abariki kolabo na Best Naso

0

Flavour-BN-2015-1BAADA ya meneja wa staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Best Naso kuwasiliana na uongozi wa staa wa muziki kutoka Nigeria, Mr Flavour, good newz ni kwamba, staa huyo amebariki kufanya naye kolabo.

Akichati na Showbiz Xtra kwa njia ya WhatsApp moja kwa moja kutoka Nigeria, Meneja wa Best Naso, Hamis Kibiti ‘Mbaba’ alisema kila kitu kinakwenda sawa na wamelazi-mika kumtafuta msanii huyo kwa kuwa mashabiki wengi wa Best Naso wamekuwa wakimfananisha naye kwa muonekano hadi kuimba.

“Mr Flavour ni msanii mtulivu na muelewa, anaukubali sana Muziki wa Bongo Fleva na niwaambie tu mashabiki wa Best Naso sasa watakuwa wamepata kile kitu walichokuwa wakikitamani kifanyike,” alisema Mbaba.

Best Naso alishawahi kubamba na ngoma kibao kama Yana Mwisho, Narudi Morogoro, Maisha Utata, Umedata, Rumba na sasa anabamba na Ukweli Upo Wapi.

CREDIT: GAZETI LA AMANI

Leave A Reply