Mr Uwazi agawa zawadi Dar

1.
Mr Uwazi akimkabidhi zawadi msomaji wa Gazeti la Uwazi Mizengwe eneo la Kituo cha Daladala cha Kigogo Freshi-Chanika.

2Msomaji wa Gazeti la Uwazi Mizengwe akipozi na Mr Uwazi kabla ya kukabidhiwa zawadi yake eneo la Chanika Mwisho.

3Wasomaji wa Gazeti la Uwazi Mizengwe sambamba na Gazeti la Ijumaa, wakiwa katika picha ya pamoja na Mr Uwazi katika Kituo cha Chanika.

4Msomaji wa Gazeti la Uwazi Mizengwe wa eneo la Mbande akipokea zawadi kutoka kwa Mr Uwazi.

5Mr Uwazi akimpatia zawadi msomaji wa Gazeti la Uwazi Mizengwe eneo la Chamazi, anayeshudia (kushoto) ni Ofisa Usambazaji wa Global, Yohana Mkanda.

6Wapenzi wasomaji wa Gazeti la Uwazi Mizengwe katika pozi na Mr Uwazi.

7Mr Uwazi akimkabidhi zawadi msomaji wa Gazeti la Uwazi Mizengwe aliyekutwa akisoma gazeti hilo eneo la Chamanzi.

8Msomaji wa Gazeti la Uwazi Mizengwe eneo la Mbagala Zakhem akikabidhiwa zawadi yake na Mr Uwazi.

9Msomaji pande za Mbagala Zakhem akipokea zawadi yake kutoka kwa Mr Uwazi Mizengwe.

ZOEZI linaloendelea la kugawa zawadi kwa wasomaji wake katika maeneo tofauti katika jijini Dar es Salaam, leo Mr Uwazi alitembelea maeneo mbalimbali ya nje kidogo ya Jiji la Dar na kugawa zawadi mbalimbali, ikiwemo sukari kwa wasomaji wa Gazeti la Uwazi Mizengwe.

Maeneo aliyotembelea Mr Uwazi ni Kigogo Freshi- Chanika, Mbande, Chamanzi na Mbagala Zakhem ambapo wasomaji wengi wa Gazeti la Uwazi Mizengwe walionekana kufurahia kutembelewa na Mr Uwazi.

Katika matembezi hayo, Mr Uwazi aliambatana na Ofisa Usambazaji wa Global Publishers, Yohana Mkanda ambaye naye alipokea maoni ya wasomaji waliokutwa wakisoma gazeti hilo.

“Zoezi kubwa la Mr Uwazi ni kuhakikisha anatoa zawadi kwa wasomaji wote kila atakapotembelea na akikuta yeyote akisoma Gazeti la Uwazi Mizengwe linalotoka kila Ijumaa, atajipatia zawadi,” alsema Mkanda.

NA DENIS MTIMA/GPL


Loading...

Toa comment